Mke wa Rais wa Jamuhuriya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli ametoa msaada wa futari kwa vituonane vya watoto yatima vilivyopo Jijini Dar es Salaam mahsusi kwa ajili yakipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Mama Magufuli ametoamsaada huo leo Jijini hapa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingiramagumu vikiwemo vya Newlife, Charambe Islamic Centre, Chakuwama, MwandaliwaYatima Centre, Al Madina Children Home, Alzam Orphanage Centre, Hiari OrphanageCentre pamoja na Ijangozaidia Orphanage Centre.
Aidha alisema kuwamsaada huo alioutoa umejumuisha Sukari mifuko 100 yenye jumla ya Kilogramu2000, Mchele mifuko 40 yenye jumla ya Kilogramu 2000 pamoja na Tende pakiti 100zenye jumla ya Kilogramu 800.
“Ninayo furaha kuwezakuwasaidia zaidi ya watoto yatima 600 ambao wamenuia kufunga katika mwezi huuMtukufu wa Ramadhani ikiwa ni muendelezo wa huduma za kujitolea kwa jamii kwakuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea Watoto yatima”, alisemaMama Magufuli.
Mke huyo wa Raisalifafanua kuwa kituo cha Newlife chenye watoto 121 kimepewa Mchele kilo 363,Sukari Kilo 363 na Tende Kilo 144, Charambe Islamic Centre chenye Watoto 54kimepewa Mchele Kilo 162, Sukari Kilo 162 na Tende Kilo 64, Chakuwama chenyeWatoto 64 kimepewa Mchele Kilo 192, Sukari Kilo 192 na Tende Kilo 64 na AlMadina Children Home chenye Watoto 65 kimepewa Mchele Kilo 195, Sukari Kilo 195na Tende Kilo 64 .
Vituo vingine niMwandaliwa Yatima Centre chenye Watoto 94 kimepewa Mchele Kilo 282, Sukari Kilo282 na Tende Kilo 64, Alzam Orphanage Centre chenye Watoto 51 kimepewa McheleKilo 153, Sukari Kilo 153 na Tende Kilo 64, Hiari Orphanage Centre chenyeWatoto 41 kimepewa Mchele Kilo 123, Sukari Kilo 123 na Tende Kilo 40 pamoja naIjangozaidia Orphanage Centre chenye Watoto 103 kimepewa Mchele Kilo 309,Sukari Kilo 309 na Tende Kilo 104.
Kwa upande wakemwakilishi wa viongozi wa vituo vya kulelea watoto yatima, Mama Kuluthum Jumaalisema kulea watoto yatima si jambo la mtu mmoja au Serikali peke yake hivyoni lazima wananchi wote wajumuike katika kuwasaidia watoto hao kwa hali na maliili wajione kuwa wako sawa na Watoto wengine wanaoishi na wazazi wao.
“Tunamshkuru sana Mkewa Rais, Mama Janeth Magufuli kwani msaada huu alioutoa kwetu sio mdogo nahakuna kitu kikubwa kama kutoa sadaka hivyo natoa rai kwa wananchi tujitahidikuwasaidia na kuwafariji Watoto hawa kwa sababu ni Watoto wa watu wote nahakuna aliyependa kuwa hivyo alivyo,” alisema Mama Kuluthumu.
Misaada kwa Watotoyatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni muendelezo wa huduma zakujitolea kwa Jamii anazofanya Mke wa Rais ambazo hufanyika kila mwaka.
Mwisho.
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO