• Wasiliana Nasi
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Baruapepe za Watumishi
    • Malalamiko
Idara ya Habari MAELEZO
Idara ya Habari MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Idara ya Habari MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Uchumi wa Tanzania Kuendelea Kupaa katika kipindi kifupi kijacho- IMF

Posted on: March 6th, 2020

Na.Mwandishi  Maalum – Dar es Salaam

Jitihada za makusudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kusimamia na kutekeleza sera madhubuti za fedha na uchumi hasa katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, pamoja na usimamizi wa Benki, zimeelezwa kuwa ni miongoni mwa vitu vilivyoifanya Tanzania kukua kiuchumi na kunakoisaidia kue ndelea na ukuaji wa kasi katika siku zijazo.

Kwa mujibu wa ripoti ndogo iliyotolewa Jijini Dar es Salaam na wataalam wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF), waliomaliza muda wao wa kufanya utafiti hapa nchini kuanzia tarehe 20 Februari hadi Machi 4 Mwaka huu, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zinazofanya vizuri katika ukuaji wa Uchumi.

Kiongozi wa timu hiyo ya IMF iliyotembelea Tanzania Enrique Gelbard  amesema kiwango cha ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miezi michache iliyopita kinaonyesha ukuaji wa kasi kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali , kuongezeka kwa mauzo ya nje ya nchi, pamoja na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi.

Amesema viashiria hivyo vitaifanya Tanzania kuendelea kukua kiuchumi katika siku zijazo katika sekta za Ujenzi na madini, unaosaidiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa kiwango cha asilimia 3.7 pamoja na kuimarika kwa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni ,kadhalika na uwepo wa akiba ya kutosha ya fedha za kigeni inayoweza kufanya manunuzi kwa kipindi cha takribani miezi mitano.

Aidha mtaalam huyo amezungumzia kuimarika kwa uchumi hapa nchini kuwa kumesababishwa na sera madhubuti za usimamizi wa fedha ambazo zimeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia amezipongeza mamlaka husika kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato.

 

Matangazo

  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Orodha ya Magazeti na Majarida ambayo Hayajahuisha Leseni ya Uchapishaji Serikalini February 05, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Tamasha la Serengeti Music and Arts Festival kufanyika Desemba 16,2020

    December 02, 2020
  • Serikali kutoa suluhu la Mawakala wa Usambazaji wa Muziki katika “Digital Platform”

    December 02, 2020
  • Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

    November 05, 2020
  • Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

    November 05, 2020
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: 25 Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@habari.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2017/18
  • Tamko la Serikali kuhusu Matumizi ya Picha za Marais Wastaafu katika Sakata la Usafirishaji wa Mchanga wa Madini
  • Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akifungua mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Mitaa Tanzania (ALAT)
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • MAELEZO PODCASTS 2020

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2019 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.