• Wasiliana Nasi
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Baruapepe za Watumishi
    • Malalamiko
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo IDARA YA HABARI-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Profile

Dkt Hassan Abbasi
Mkurugenzi wa Idara ya Habari

Dkt Hassan Abbasi ambaye ndiye Mkurugenzi wa sasa wa Idara ya Habari-MAELEZO alizaliwa wilayani Korogwe, Tanga mwaka 1978 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Hale kati ya mwaka 1988 na 1994. Alimaliza akiwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri mkoani humo na kujiunga na Sekondari ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Tabora Wavulana (Tabora School) mwaka 1995 kwa masomo ya sekondari.  


Kati ya mwaka 1997 na 1998 alihamia katika Sekondari ya Azania, Dar es Salaam ambapo alimaliza kidato cha nne na kati ya mwaka 1999-2001 alijiunga na Shule ya Sekondari Lindi kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Kati ya mwaka 2002 na 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua shahada ya kwanza ya sheria (LL.B). Akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu pia aliajiriwa kama mwandashi wa habari wa kujitegemea katika kampuni ya Business Times na baadaye kushika nafasi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi, mhariri msaidizi hadi mhariri mkuu katika magazeti ya Majira na Kulikoni.

Mwaka 2005 akiwa bado mwanafunzi, alichaguliwa kuwa Mhariri Mkuu wa Jarida liitwalo “Nyerere Law Journal” linalochapishwa na Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kati ya mwaka 2007 na 2008 alihudhuria masomo ya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi ikiwemo makao makuu ya Reuters, London, Uingereza na Chuo Kikuu cha Maine nchini Marekani.

Mwaka 2010 aliajiriwa Serikalini akiwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) tawi la Tanzania, programu iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Nje kabla ya mwaka 2014 kuwa Meneja Mawasiliano katika Ofisi ya Rais, Kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Agosti 5, 2016. Pamoja na taaluma ya sheria ambako ana hadhi ya Wakili wa Mahakama Kuu tangu mwaka 2011,  Dkt. Abbasi pia ana diploma ya uzamili katika usimamizi wa mahusiano ya kimataifa (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia cha Msumbiji na Tanzania, Kurasini, shahada ya uzamili katika mawasiliano kwa umma (MA Mass. Comm., SAUT) na shahada ya uzamivu katika mawasiliano kwa umma (Ph.D Mass. Comm., SAUT).

Matangazo

  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Orodha ya Magazeti na Majarida ambayo Hayajahuisha Leseni ya Uchapishaji Serikalini February 05, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais Magufuli atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa

    November 21, 2019
  • Rais Magufuli azindua Kitabu cha Maisha binafsi ya Rais Msaafu Benjamin Mkapa

    November 12, 2019
  • Rais Magufuli akutana na viongozi wa AALCO

    October 24, 2019
  • Afrika ni muhimu kwa Maendeleo ya Uchumi wa Dunia- Putin

    October 24, 2019
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: 25 Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@habari.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2017/18
  • Tamko la Serikali kuhusu Matumizi ya Picha za Marais Wastaafu katika Sakata la Usafirishaji wa Mchanga wa Madini
  • Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akifungua mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Mitaa Tanzania (ALAT)
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2019 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.