Kwa niaba ya watumishi wa Idara ya Habari-MAELEZO, ninayo furaha kukukaribisha katika tovuti hii. Tunatumaini utapata taarifa za kuaminika unazozihitaji kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa mamlaka, dira, dhamira, malengo, mikakati, shughuli kuu, ahadi na utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Ujio wa tovuti hii ni tukio la kihistoria katika kufikia dira na matarajio yetu hasa kutangaza shughuli za Serikali lakini pia na huduma zetu kwa umma.
Kupitia tovuti hii tunaamini kwamba itakuwa rahisi kwa wananchi kupata taarifa. Ni matumaini yangu kuwa kila atayetembelea tovuti hii atapata jambo la kumfurahisha, kumfundisha au kumuelimisha.
Ni nia yetu kuendelea kuboresha tovuti hii kadri muda unavyokwenda ili ipatikane kwa urahisi na ubora wa hali ya juu. Tunafurahi sana kuzungumza na watembeleaji wa tovuti waliohamasika na tunathamini kila maoni tutakayoyapokea.
Karibuni sana.
Idara ya Habari- MAELEZO.
Hakimiliki ©2019 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.