Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

HUDUMA ZETU

Fahamu baadhi ya Huduma Zetu!

Idara ya Habari-MAELEZO ina jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na Miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya sera na sheria za habari.

Taratibu za leseni

Masharti Ya Utoaji Leseni Kwa Magazeti/Majarida

  • Cheti cha Usajili wa Kampuni/Taasisi au aina nyingine ya Usajili wa kisheria (Kwa taasisi za Serikali barua kutoka kwa Mtendaji Mkuu);
  • Andiko la mradi wa gazeti/jarida linalojumuisha Dira, Dhima, Será ya Gazeti/Jarida husika, mahali/eneo la kufanyia biashara, wasifu binafsi (CV) na vyeti vya taaluma vya Mhariri na Waandishi;
  • Mfano wa muundo/mwonekano wa gazeti/jarida (dummy); na
  • Malipo ya ada kama yalivyoanishwa katika kanuni (TZS 1,000,000/ [Shilingi Milioni Moja Tu])

ZINGATIA: Malipo yote kwa ajili ya usajili yatafanyika katika ofisi za MAELEZO Dar es Salaam au Dodoma.