Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.
TAARIFA HII NI FEKI (SEPTEMBA 08, 2026)
Ipuuzeni taarifa hii ya uzushi iliyotengenezwa na wahalifu.Tunawasisitiza Watanzania kuendelea kufuatilia taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi ikiwemo tovuti ya Idara ya Habari MAELEZO (www.maelezo.go.tz) na akaunti za Idara ya Habari MAELEZO kwenye mitandao ya kijamii (Msemaji Mkuu wa Serikali au Maelezo News).
TUHUMA HIZI HAZINA UKWELI (AGOSTI 16, 2026)
Serikali ya Tanzania imezisikia tuhuma zisizo za kweli kutoka kwa mgombea Urais wa chama cha NRPUP nchini Zambia, Bw. Brian Mundubile, kwamba Tanzania imetuma watu kwenda nchini Zambia kwa lengo la kuingiliana kuvuruga uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026.
Serikali imezichukulia kwa uzito tuhuma hizo na kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia imeiandikia Serikali ya Zambia kutaka maelezo ya kina juu ya kwa nini mgombea huyu amezusha tuhuma hizo zisizo na ukweli. Serikali ya Tanzania inawahakikishia Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa haijatuma mtu yeyote kuingilia au kuvuruga uchaguzi wa Zambia na haina utamaduni huo.
Kama ilivyo kwa nchi zingine za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Tanzania inao uwakilishi wa waangalizi wa uchaguzi huo ambao wanafanya kazi kulingana na miongozo ya waangalizi wa uchaguzi wa SADC sambamba na waangalizi wengine waliopo Zambia na sio kuingilia uchaguzi kama ilivyotuhumiwa na Bw. Brian Mundubile.
The Government of Tanzania is concerned with the false allegations made by the NRPUP Presidential Candidate in Zambia, Mr. Brian Mundubile, claiming that Tanzania sent individuals to Zambia with the intention of interfering with and disrupting the country’s general elections held on 13th August 2026.
The Government takes these allegations seriously and through the Tanzanian High Commission in Zambia, has written to the Government of Zambia seeking detailed clarification on the basis upon which the candidate made these unfounded allegations.
The Government of Tanzania wishes to reassure Tanzanians and the international community that it has not sent anyone to interfere with or disrupt Zambia’s elections and has no such practice. As is the case with other member states of the Southern African Development Community (SADC), Tanzania has a representation of election observers in Zambia who are carrying out their duties in accordance with SADC election observation guidelines, alongside other observers present in Zambia. Their role is to observe the electoral process and not to interfere in the elections, as alleged by Mr. Brian Mundubile.
PUUZENI UPOTOSHAJI HUU (AGOSTI 14, 2026)
Video hii inasambazwa kwa lengo ovu la kupotosha wananchi na kuichafua Serikali. Hakuna mradi wa maji uliojengwa kwa lengo la kusambaza maji ya tope kama haya. Inaweza kutokea mara chache wakati wa usafishaji wa miundombinu ya maji au kama kuna tatizo katika njia za maji zinazopita ardhini na hutatuliwa mara Mamlaka za Maji zinapopata taarifa. Wapuuzeni WAPOTOSHAJI na WACHOCHEZI wenye malengo maovu.
PICHA HII IMEHARIRIWA KWA AKILI UNDE (AI), IPUUZWE (JULAI 11, 2026)
Picha hii imetengenezwa kwa makusudi ikiwa na nia ovu yakupotosha watanzania na kuharibu taswira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukio halisi (Picha ya chini) lilitokea Disemba 13. 2023, wakati Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Millenia (MCC), Bi. Alice Albright, kwa njia ya mtandao kutokea lkulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
BARUA HII NI FEKI (JULAI 1, 2026)
Puuzeni barua hii ambayo imetengenezwa na wahalifu kwa nia ovu. Hakuna mabadiliko ya tarehe za kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari. Shule zote zitafunguliwa kwa tarehe zilizopangwa.
UPOTOSHAJI: VIDEO HII NI FEKI! (JUNI 16, 2026)
Puuzeni video hii iliyotengenezwa kwa akili unde (AI) na watu wenye nia ovu dhidi ya nchi yetu. Wahalifu wanasambaza video hii kupitia mitandao ya kijamii ili kuhamasisha watu kushiriki vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na kuharibu mali ikiwemo miundombinu ya umma na biashara za watu.
Serikali inatoa wito kwa wananchi kupuuza kampeni kama hizi na kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama pale mtakapobaini watu wanaohamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani.
UPOTOSHAJI: TAARIFA HII IMEPOTOSHWA! (JUNI 10, 2026)
Hakuna zuio la aina hiyo kwa watengeneza maudhui hawa wala wengine wowote kutoka nchi yoyote duniani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya kazi kwa karibu na watengeneza maudhui wote na Tanzania inawakaribisha nchini. Habari hii imepotoshwa na ina nia yakutengeneza taharuki.
UPOTOSHAJI: TAARIFA FEKI! (MEI 22, 2026)
Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, hajazungumza maneno haya mahali popote. Upotoshaji huu umetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu uhusiano mzuri uliyopo kati ya Tanzania na wadau wa utalii. Kwa taarifa sahihi kutoka Idara ya Habari MAELEZO tembelea tovuti (www.maelezo.go.tz) na mitandao ya kijamii ya Idara ya Habari (Msemaji Mkuu wa Serikali/Maelezo News).
UPOTOSHAJI: TAARIFA HII NI YA NOVEMBA 26, 2025 (MEI 12, 2026)
Puuzeni upotoshaji huu. Bunge la Ulaya haliendeshi mjadala huu kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanaojiita wanaharakati mtandaoni. Video hii ni ya Novemba 26, 2025 na hakuna maazimio haya dhidi ya Tanzania. Serikali inaendelea kuwasihi watanzania kuepukana na usambazaji wa taarifa hizi zenye lengo la kuzua taharuki na kuchochea chuki. IPUUZWE!
TAARIFA FEKI: MHESHIMIWA RAIS SAMIA HAJAZUNGUMZA MANENO HAYA! (MEI 10, 2026)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hajazungumza maneno haya. Taarifa hii imetengenezwa kwa lengo la kupotosha umma na kuharibu uhusiano mzuri uliyopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. IPUUZWE!
TAARIFA FEKI: MHESHIMIWA RAIS SAMIA HAJASEMA MANENO HAYA (MACHI 12, 2026)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hajatamka maneno haya. Uzushi huu unatengenezwa na wenye nia ovu. WAPUUZWE!
HAWA NI MATAPELI: HAKUNA MKOPO WA NAMNA HII (MACHI 4, 2026)
Jitahadharini na matapeli. Hakuna mikopo ya namna hii inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wala Serikali.
Thibitisha / Fact Check