Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.
UPOTOSHAJI: VIDEO HII NI FEKI!
Puuzeni video hii iliyotengenezwa kwa akili unde (AI) na watu wenye nia ovu dhidi ya nchi yetu. Wahalifu wanasambaza video hii kupitia mitandao ya kijamii ili kuhamasisha watu kushiriki vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na kuharibu mali ikiwemo miundombinu ya umma na biashara za watu.
Serikali inatoa wito kwa wananchi kupuuza kampeni kama hizi na kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama pale mtakapobaini watu wanaohamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani.
UPOTOSHAJI: TAARIFA HII IMEPOTOSHWA!
Hakuna zuio la aina hiyo kwa watengeneza maudhui hawa wala wengine wowote kutoka nchi yoyote duniani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya kazi kwa karibu na watengeneza maudhui wote na Tanzania inawakaribisha nchini. Habari hii imepotoshwa na ina nia yakutengeneza taharuki.
UPOTOSHAJI: TAARIFA FEKI!
Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, hajazungumza maneno haya mahali popote. Upotoshaji huu umetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu uhusiano mzuri uliyopo kati ya Tanzania na wadau wa utalii. Kwa taarifa sahihi kutoka Idara ya Habari MAELEZO tembelea tovuti (www.maelezo.go.tz) na mitandao ya kijamii ya Idara ya Habari (Msemaji Mkuu wa Serikali/Maelezo News).
UPOTOSHAJI: TAARIFA HII NI YA NOVEMBA 26, 2025
Puuzeni upotoshaji huu. Bunge la Ulaya haliendeshi mjadala huu kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanaojiita wanaharakati mtandaoni. Video hii ni ya Novemba 26, 2025 na hakuna maazimio haya dhidi ya Tanzania. Serikali inaendelea kuwasihi watanzania kuepukana na usambazaji wa taarifa hizi zenye lengo la kuzua taharuki na kuchochea chuki. IPUUZWE!
TAARIFA FEKI: MHESHIMIWA RAIS SAMIA HAJAZUNGUMZA MANENO HAYA!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hajazungumza maneno haya. Taarifa hii imetengenezwa kwa lengo la kupotosha umma na kuharibu uhusiano mzuri uliyopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. IPUUZWE!
TAARIFA FEKI: MHESHIMIWA RAIS SAMIA HAJASEMA MANENO HAYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hajatamka maneno haya. Uzushi huu unatengenezwa na wenye nia ovu. WAPUUZWE!
HAWA NI MATAPELI: HAKUNA MKOPO WA NAMNA HII
Jitahadharini na matapeli. Hakuna mikopo ya namna hii inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wala Serikali.
Thibitisha / Fact Check