Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

Na Scolastica Sambi – MAELEZO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani kuongeza nguvu katika utoaji wa haki nchini na kuwasisitiza kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa kwa mustakabali wa Taifa na ustawi wa wananchi. Akizungumza wakati wa kuwaapisha majaji hao, tarehe 26 Mei, 2026, Ikulu Dar es Salaam, Rais, Dkt. Samia amesema uteuzi wao umetokana na uzoefu, weledi pamoja na utumishi mzuri waliouonyesha katika nafasi mbalimbali walizowahi kuzitumikia ndani ya mhimili wa Mahakama.   Amesema hatua ya kupandishwa kwao ni ishara kuwa kazi zao zimetambuliwa na kuthaminiwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama, jambo linaloonyesha imani kubwa waliyopewa katika kusimamia haki za Watanzania. “Nendeni mkatumikie nchi kwa uadilifu, weledi na uzalendo kama mlivyoapa hapa. Dhamana hii si ya cheo tu, bali ni wajibu wa kulinda haki za wananchi,” amesema Rais Samia. Katika hotuba yake, Rais Samia amesema kazi ya jaji ni miongoni mwa majukumu yenye uzito mkubwa katika jamii kwa sababu ndiyo yanayogusa moja kwa moja maisha, haki na matumaini ya wananchi. “Ukimuacha Mungu anayesimamia haki za wote, basi wengine aliowateua kusimamia haki za wananchi ni ninyi majaji. Hivyo mnafanya kazi yenye dhamana kubwa kwa Taifa,” amesisitiza. Aidha, aliwataka majaji hao kuhakikisha wanaitunza heshima na uhuru wa mahakama kwa kutoa maamuzi yanayozingatia sheria, haki pamoja na maslahi mapana ya Taifa, huku akieleza kuwa Mahakama ya Rufani ndiyo ngazi ya juu kabisa ya utoaji haki nchini. Rais Samia ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mhimili wa mahakama kupitia maboresho mbalimbali ili kuhakikisha taasisi hiyo muhimu inaendelea kutoa haki kwa ufanisi, weledi na kwa wakati.

By Baraka Messa – MAELEZO Former Manchester United and England defender Rio Ferdinand has praised Tanzania’s investment in sports infrastructure, describing the country’s hospitality and commitment to sports development as exceptional. Speaking on May 21 during a visit to the ongoing construction of the Arusha Sports Complex, Ferdinand said he was impressed by the warm reception he had received since arriving in Tanzania, adding that he had rarely experienced such hospitality elsewhere in the world. “ The reception I have received in Tanzania has been truly special. The people are very welcoming, the food is excellent and, overall, Tanzania is a beautiful country,” Ferdinand said. The former football star said every place he had visited in Tanzania was marked by warmth, respect and generosity from local residents, making him feel at home. Ferdinand added that the hospitality he experienced had encouraged him to return to the country and strengthen cooperation with Tanzania in the development of sports. He also commended progress on the construction of the Arusha Sports Complex, describing it as one of the most impressive modern sporting facilities he had seen and a reflection of Tanzania’s commitment to advancing the sports sector. “I have played in many stadiums around the world, but this facility stands out for its quality and modern standards. I congratulate the builders, contractors and all experts involved in implementing this important project,” he said. Ferdinand said he plans to return to Tanzania once the stadium is completed to witness its impact firsthand, noting that investment in modern sports facilities is essential for nurturing talent and promoting the growth of football in the country.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa, amesema kuwa ujio wa wanamichezo wa kimataifa nchini Tanzania akiwemo mchezaji na nahodha wa zamani wa Klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, Rio Ferdinand unashawishi wawekezaji kuwekeza katika sekta hiyo. Bw. Msigwa ameeleza hayo Mei 20, 2026 wakati akiwa safarini na mwanamichezo huyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa kutumia treni ya Reli ya Kisasa (SGR) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake nchini. Ameongeza  kuwa wachezaji wa kimataifa wanapokuja nchini wanaongeza macho ya wadau mbalimbali wa michezo kuitazama nchi ya Tanzania na kuona ni namna gani wataweza kuwekeza  na nchi itaweza kunufaika kwa kupata mitaji ya kuwekeza kwenye michezo, wataalam wa kushirikiana nao pamoja na kutengeneza fursa kwa vijana kunufaika na fursa ziliozopo duniani kupitia sekta hiyo. “Ujio wa mwanamichezo huyu, unapeleka ujumbe duniani kwamba Tanzania imejidhatiti kufanya mambo makubwa kwenye sekta ya michezo hivyo kupitia wao, nchi itafanikiwa kushawishi uwekezaji katika sekta ya michezo kwani nchi yetu ina changamoto kubwa kwenye eneo la uwekezaji hasa kwenye miundombinu ya michezo pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo jezi za wachezaji, viatu, mipira ambavyo tunaagiza kutoka nje. Vile vile, tunahitaji wataalam wa michezo ambao wataleta ujuzi wa namna ya kutengeneza viwanja.” Amesema Msigwa. Kwa upande wake, Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, Rio Ferdinand amesema kuwa mpira wa miguu ukitumika vizuri unaweza kufungua fursa mbalimbali pamoja na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.  Amesema kuwa anaendelea kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda pamoja na wadau wa sekta ya utalii ili kuongeza hamasa na ufuatiliaji wa sekta hiyo.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, amesema kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), linatarajia kuanza safari za ndege kuelekea nchini Urusi mnamo Juni, 2026. Ameyasema hayo Mei 15, 2026 jijini Arusha wakati aliposhiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi linaloendelea jijini humo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Waziri Mahmoud ameeleza kuwa, nchi ya Urusi inapendelea kupata mazao yenye viwango vya hali ya juu kutoka nchini Tanzania lakini huenda ni ngumu wafanyabiashara kukidhi kigezo hicho kutokana na uhaba wa usafiri wa haraka wa kufikisha bidhaa zikiwa na ubora wake. “Tunalishukuru shirika letu la ndege nchini kwa kukamilisha mikataba yote ambapo ifikapo Juni 2026, safari zitaanza kutoka Tanzania kwenda jijini Moscow na baadaye Saint Petersburg. Wakati ndege hizo zinarudi kutoka kwenye maeneo hayo, tunategemea zitabeba watalii watakaokuja kufanya utalii nchini katika maeneo ya Zanzibar, Kilimanjaro na Dar es Salaam”. Ameongeza kuwa, shirika hilo litakuwa na ndege itakayobeba mizigo hivyo, ametoa rai kwa wafanyabiashara wanaohitaji kusafirisha bidhaa kwa haraka kutumia usafiri huo. Ametaja baadhi ya fursa ambazo Tanzania na Urusi wanaweza kushirikiana ikiwemo ujenzi wa viwanda vya mbolea, vifaa vya kilimo, shughuli za ufungashaji, usindikaji na uhifadhi wa bidhaa, TEHAMA pamoja na dawa za binadamu.

Na Mwandishi Wetu Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amewaomba Watanzania kuendelea kulinda na kuitunza amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa wapo baadhi ya watu wanaotumika kuhamasisha vurugu nchini, hivyo ni muhimu kuwakataa kwani ustawi na maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya Taifa hayawezekani pasipokuwa na amani na utulivu. Msigwa amebainisha hayo leo Jumapili Mei 10, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Njombe kwenye shamba la muwekezaji wa zao la Parachichi pembezoni mwa Mji wa Njombe, akiwapongeza pia Watanzania kwa kuwakataa wale wanaohamasisha vurugu Nchini na kusisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kujielekeza katika habari zenye kuleta maendeleo na kuhamasisha umuhimu wa amani Nchini. “Najua maneno yapo mengi na wahamasishaji wamekuwa wengi. Mwalimu Nyerere alishatuambia kuwa mabeberu hawajalala na pia wakati mwingine wanawatumia miongoni mwa Watanzania kufikia malengo yao. Tuamke, hakuna nchi iliyofanikiwa kupata maendeleo ikiwa watu wake wanavurugana, wanagombana, wapo kwenye maandamano kila siku na kuhamasishana kuchoma miundombinu au kuharibu uchumi. Tukifika huko hatutatoboa.” “Nawaombeni ndugu zangu Watanzania tulinde amani yetu kwa wivu mkubwa, tukatae hamasa zozote zinazoashiria fujo na vurugu kwenye Nchi yetu. Tuwakatae wanaohamasisha vurugu na ninajua Watanzania wengi wamekataa na niwapongeze sana kwa hilo.”amesema Msigwa. Katika hatua nyingine, Msigwa pia amewataka Maafisa habari kote nchini kutenga muda na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza amani, utulivu na mshikamano wa Watanzania kama msingi wa kuweza kutekeleza Dira 2050 pamoja na hatua nyingine za maendeleo na ustawi wa jamii.