Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

Mapacha Watano Wazaliwa Muhimbili: Serikali Kugharamia Matibabu

June 13, 2026

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeandika historia nyingine baada ya jopo la madaktari bingwa na wataalamu wa afya kufanikisha salama uzazi wa watoto watano kwa wakati mmoja kwa Bi. Victoria Mkwizu, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam.

Watoto hao ambao watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike, wamezaliwa tarehe 13 Juni 2026 na wanaendelea vizuri chini ya uangalizi wa wataalamu wa hospitali hiyo.

Akiwa wodini, Bi. Victoria amesema anafurahia huduma alizopata katika hospitali hiyo tangu alipopokelewa hadi kujifungua.

“Nawapongeza madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa afya kwa uangalizi wa karibu walionipatia katika kipindi chote cha matibabu kwani mchango wao umetuwezesha mimi na watoto kuendelea vizuri”, amesema Bi. Victoria.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dkt. Rachel Mhaville amesema tukio hilo ni la kipekee na limehitaji ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa timu ya wataalamu wa hospitali hiyo ili kuhakikisha usalama wa mama na watoto huku akimpongeza Bi. Victoria kwa kujifungua salama na kuwatakia wote afya njema.

Tunampongeza sana Bi. Veronica kwa kubarikiwa watoto mapacha watano, hospitali yetu itagharamia gharama zote za matibabu za kwake na watoto wake kuanzia alipolazwa hospitalini tarehe 15 Mei, 2026 hadi watakapomaliza matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani”, ameeleza Dkt. Rachel.

Amefafanua kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za hospitali kuhakikisha mama na watoto wanaendelea kupata huduma bora na salama katika kipindi hicho.

Bingwa Bobezi wa Watoto Wachanga na Mkuu wa Kitengo cha Wadi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Martha Franklin Mkonyi, akimuhudumia mmoja wa watoto watano waliozaliwa hospitalini hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *