Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

Rais Samia atoa Ndege kuwachukua Serengeti Boys

June 2, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa ndege maalum kwa ajili ya kuwachukua mashujaa, Timu ya Taifa ya Vijana U-17 (Serengeti Boys) baada ya kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON U-17, 2026.

Ndege hiyo imeondoka Juni 01, 2026 inatarajiwa kurejea Jumatano tarehe 3 Juni 2026.

Msafara huo umeongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb.), akiambatana na viongozi wa serikali pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) ambao watatumia fursa hiyo kushiriki mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu zilizopo kwenye kalenda ya FIFA, kama sehemu ya maandalizi ya mashindano yajayo.

Aidha, Waziri Makonda amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza kwenye michezo na kurahisisha safari hii. Ameziomba familia za Watanzania kuungana kuiombea na kuishangilia Serengeti Boys ili wailetee nchi Kombe la AFCON U-17 na kupeperusha bendera yetu kimataifa.

No Next Post Available

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *