AFCON 2027 Kuchochea Ajira na Kukuza Biashara Afrika Mashariki
Na Josephina Lupasha – MAELEZO
Serikali imewataka Watanzania kutumia mashindano ya AFCON 2027 kama fursa ya kujenga uchumi kupata ajira, kufanya biashara na uwekezaji badala ya kulichukulia kama tukio la michezo pekee.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi za Sekretarieti ya AFCON zilizohamishiwa nchini Tanzania, katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Novemba 25, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema mafanikio ya mashindano ya AFCON hayatapimwa kwa idadi ya mabao yatakayofungwa, ukubwa wa viwanja au shangwe za mashabiki pekee, bali kwa manufaa yatakayopatikana kwa wananchi, zikiwemo ajira zitakazozalishwa, biashara zitakazokua, ongezeko la watalii na maboresho yatakayochochea maendeleo ya maisha yao.
Mfanikio yetu hayatapimwa kwa ukubwa wa viwanja pekee, idadi ya mabao yatakayofungwa au ukubwa wa shangwe za mashabiki yatapimwa kwa idadi ya ajira, biashara , watalii tutakaowavutia na maisha ya wananchi tutakayyabadilisha.
Amesisitiza kuwa, wafanyabiashara wanapaswa kujipanga kwa kupanua huduma zao, kusajili biashara, kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali na kuwekeza katika lugha za kimataifa ili kuwasiliana na wageni hususani wakati wa biashara na utoaji wa huduma.
Sambamba na hayo, Waziri Makonda amesema maandalizi ya AFCON yanapaswa kwenda sambamba na ujenzi wa uchumi ili fursa zitakazotokana na mashindano hayo ziwanufaishe wananchi kwa muda mrefu.