Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

Arusha kuwa Lango la Fursa

November 19, 2026

Na Bupe Mwaiseje – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Mkoa wa Arusha unatarajiwa kuwa kitovu cha mikutano ya kimataifa, hali itakayofungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi kupitia biashara na sekta ya utalii.

Akizungumza na wananchi wa Arusha Novemba 19, 2026 jijini Arusha, amesema ujio wa watu kutoka mataifa mbalimbali utaiweka Arusha katika nafasi muhimu ya kupokea wageni watakaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali, huku wakipata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii, ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine.

Nawaombeni sana hiyo ni fursa itumieeni, kama mlivyotumia fursa zilizopita na hii ni fursa itumieeni.

Amebainisha kuwa wananchi wa Arusha, wanatakiwa kutumia fursa hiyo kujinufaisha kiuchumi, akieleza kuwa wamiliki wa hoteli, wafanyabiashara wadogo na wadau wa utalii watanufaika kutokana na ongezeko la wageni na mzunguko wa fedha.

Vile vile, amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu, akiwataka wananchi kuhakikisha wageni watakaofika nchini wanapata mazingira salama ya kushiriki katika shughuli zao mbalimbali kuondoka salama.

Aidha, amewataka viongozi na wananchi kuhakikisha Arusha inakuwa safi na yenye mazingira mazuri, ili wageni watakaofika waondoke na taswira nzuri ya Tanzania.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amewahakikishia wananchi wa Arumeru kuwa Serikali itashughulikia changamoto ya upatikanaji wa maji, akisema kuwa amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuhusu tatizo hilo na kupata maelezo kuhusu changamoto ya mgawanyo wa maji kutoka chanzo cha Mtikane.

Hata hivyo, amesema kuwa suala hilo linapatiwa ufumbuzi na Serikali itahakikisha maji yanawafikia wananchi wa Arumeru na maeneo mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *