Karibu!

Tunakukaribisha kwenye tovuti rasmi ya Msemaji Mkuu wa Serikali upate taarifa na habari sahihi zenye kuakisi malengo ya Serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na matarajio ya Watanzania.

Mawasiliano

Tufuatilie

Makamu wa Rais Aagiza Uchunguzi Mradi Uliotumia Bilioni 4.2 Lindi

November 14, 2026

Na Mwandishi wetu- Lindi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa kuboresha miundombinu ya Manispaa ya Lindi, baada ya taarifa kuonesha kuwa mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 4.22, huku utekelezaji ukiwa asilimia 24 na muda mkataba uliotumika ukiwa asilimia 80.

Akitoa maelekezo Novemba 14, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Lindi, Makamu wa Rais ametaka kufahamishwa namna malipo yalivyofanyika, fedha zilivyotumika na sababu za kazi kutotekelezwa kwa kasi iliyotarajiwa ambapo pia ameagiza taarifa ya uchunguzi imfikie ili aiwasilishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Ndejembi amehoji sababu za mkandarasi kuendelea kulipwa fedha nyingine wakati Halmashauri yenyewe ilieleza kuwa hakuwa na nidhamu katika matumizi ya malipo ya awali.

Aidha, ameonesha kutoridhishwa na maelezo ya halmashauri kwamba imemwandikia mkandarasi barua 16 kuhusu kusuasua kwa mradi huo akieleza kuwa Halmashauri hiyo ilipaswa kuchukua hatua badala ya kuendelea kuandikiana barua wakati fedha za umma zimeshalipwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Lindi pamoja na kuzungumza na wananchi wa Lindi katika Mkutano wa hadhara uliyofanyika Lindi mjini.

Taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa wakati wa ukaguzi wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 19.06 imeeleza kuwa mradi unatekelezwa na kampuni ya Hamerkop International Limited JV KIKIM Contractor’s Limited ambapo mkandarasi amelipwa jumla ya shilingi bilioni 4.22, zinazojumuisha malipo ya awali ya shilingi bilioni 2.86 na malipo kupitia hati namba mbili ya shilingi bilioni 1.36.

Mkataba wa mradi huo ulisainiwa Juni 25, 2025, mjini Dodoma, na kazi kuanza rasmi Novemba 7, 2025. Mradi unatakiwa kukamilika Februari 5, 2027. Kwa mujibu wa taarifa, utekelezaji ulitarajiwa kufikia asilimia 80 katika hatua hii, hivyo kiwango cha asilimia 24 kilichofikiwa kiko nyuma kwa pointi 56 za asilimia.

Mradi huo, unatekelezwa kupitia mpango wa TACTIC, unajumuisha Soko Kuu la Matopeni, barabara za kilomita 5.3, Stendi ya Mabasi Mitwero na Ofisi ya Uratibu wa Mradi. Unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Serikali chini ya TAMISEMI, huku usimamizi wa kitaalamu ukifanywa na Inter-Consult Limited kwa kushirikiana na Tanzo Vision Engineering Limited.

Kusuasua kwa ujenzi wa mradi huo kulimfanya Waziri anayehusika na TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, kufanya ukaguzi Septemba 14, 2026. Aliagiza mkandarasi atafute wakandarasi wadogo wenye uwezo, pamoja na kuundwa kwa timu maalumu ya ufuatiliaji iliyobaini mkandarasi hana uwezo wa kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa na kupedekeza abaki na ujenzi wa soko, huku kazi nyingine tatu zikitekelezwa na wakandarasi wadogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts